Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampala yajitahidi kukabili athari za majanga

Kampala yajitahidi kukabili athari za majanga

Uongozi wa mji mkuu wa Uganda , Kampala umetoa kipaumbele katika maendeleo ya miundombinu , njia za kuwekeza zinazozingatia mazingira na kupunguza uzalishaji wa hewa chafu ili kuimarisha uwezo wa mji huo kakabiliana na majanga ya asili na yanayosababishwa na binadamu. Amina Hassan na taarifa zaidi.

(TAARIFA YA AMINA)

Kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa mataigfa ya upunguzaji wa hatari ya majanga UNISDR , mamlaka ya mji wa Kampaka KCCA na washirika wa maendeleo wametenga fungu maalumu la fedha kukarabati barabra, kuboresha mifumo ya maji taka, kuimarisha mikakati ya kudhibi mabadiliko ya tabia nchi na kufufua usafiri wa umma ili kukabiliana na maafa na hatari ya majanga itokanayo na kukua haraka kwa mji.

UNISDR inasema mtazamo huo ndio kiini cha makataba wa miaka 15 wa Sedai kwa ajili ya upunguzaji majanga, uliopitishwa kimataifa mwaka 2015.

Kampala ndio kitovu cha uchumi wa Uganda , ikiwa na 80% ya shughuli ya viwanda na biashara, na ni ishara ya mabadiliko Uganda