Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID yaimarisha ulinzi baada ya mashambulizi Sortoni:

UNAMID yaimarisha ulinzi baada ya mashambulizi Sortoni:

Kufuatia mashambulizi ya wiki hii kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani na shambulio la risasi karibu na soko mjini Sortoni Kaskazini mwa Darfur na kukatili maisha ya watu watano huku likijeruhi wengine wengi, mpango wa pamoja wa Umoja wa mataifa na Muungano wa Afrika wa kulinda amani Darfur UNAMID umeimarisha ulinzi kwenye kambi hiyo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon na mwenyekiti wa tume ya muungano wa afrika Nkosazana Dlamini-Zuma wametoa wito kwa serikali ya Sudan kuchunguza na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria wahusika. Ashraf Eissa ni msemaji wa UNAMID

(SAUTI ASHRAF CUT 1)

“Tunaongeza doria hasa katika eneo hilo , tunazunguika saa 24 siku 7 za wiki, pia tunaongeza juhudi za kuwaingizia maji watu hapa ambao wana shida kubwa ya maji . Maji ni muhimu sana sio tu kwa kuendesha maisha bali pia kwa usafi na kuweka mazingira bora kwa afya haraka iwezekanavyo”

Sortoni inahifadhi wakimbizi wandani 90,000. Eissa anasema wamezitaka pande zote za mzozo kuheshimu sheria za kimataifa zinazotaka kambi za wakimbizi wa ndani kuwa huru bila silaha

(SAUTI ASHRAF CUT 2)

Wakati raia wako kwenye ulinzi wetu, wanapaswa kuwa raia kikamilifu na hakutakiwi kuwa na silaha zozote au kujihusisha na silaha kwa sababu , hilo likitokea wahanga ni wanawake na watoto ambao kwanza wametawanywa na machafuko."