Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kosovo: Licha ya hatua zilizopigwa bado kuna changamoto

Kosovo: Licha ya hatua zilizopigwa bado kuna changamoto

Baraza la usalama leo asubuhi limejadili kuhusu hali ya Kosovo. Wajumbe wamesikia taarifa ya hatua zilizopigwa nchini humo , hali kadhalika changanmoto zilizopo.

Kwa mujibu wa Zahir Tanin, mwakilishi maalumu na mkuu wa mpango wa Umoja wa mataifa Kosovo (UNMIK) amesema moja ya hatua nzuri zilizopigwa ni kufanyika kwa uchaguzi wa Rais mwezi Aprili na kuundwa kwa serikali mpya ya Serbia.

Ameongeza kuwa suala linguine ni kuimarika kwa uhusiano na Muungano wa Ulaya , huku kukitangazwa makubaliano ambaye amesema yanaweza kuwapa watu wa Kosovo amani, matumaini na mustakhbali bora suala ambalo linachagiza majadiliano baiana ya

Belgrade and Pristina. Hata hivyo ameainisha changamoto zilizopo ambazo ni

(SAUTI YA ZAHIR TANIN)

Ukosefu wa ajira, kutokuwepo usawa, ukwepaji sheria, malengo endelevu na taasisi dhaifu, ambavyo ni vikwazo kwa amani na utulivu”