Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatoa miongozo ya kuboresha huduma kwa mamilioni ya wanaoishi na ukeketaji

WHO yatoa miongozo ya kuboresha huduma kwa mamilioni ya wanaoishi na ukeketaji

Mapendekezo mapya ya shirika la afya duniani WHO yana lengo la kuwasaidia wahudu wa afya kutoa huduma bora zaidi kwa wanawake na wasichana zaidi ya milioni 200 kote duniani wanoishi na ukeketaji. Joseph Msami na taarifa zaidi

(TAARIFA YA JOSEPH MSAMI)

WHO inasema ukeketaji unafanyika bila sababu zozote za kitabibu na hauna faida kwa afya, bali unaweza kusababisha madhara makubwa na kukiuka haki za wanawake na wasichana. Ukeketaji unaweza kusababisha kutokwa damu kupita kiasi, matatizo ya kukojoa na baadaye uvimbe kwenye mirija ya uzazi, maambukizi na kifo.

Pia ukeketaji unaweza kusababisha matatizo wakati wa kujifungua na kuongeza harati ya vifo kwa watoto wachanga.

WHO imeongeza kuwa wahudumu wa afya wanahitaji kuandaliwa kwa mafunzo muafaka ili kuwahudumia waathirika hawakwani mara nyingi hawatambui athari na madhara ya ukeketaji. Dr Flavia Bustreo ni naibu mkurugenzi mkuu wa WHO

(SAUTI YA DR FLAVIA)

"Miongozi ni kwa ajili ya kila mtu anayetoa huduma kwa wasichana na wanawake, inachagiza na kusisitiza ni kwa nini hawa wanawake na wasichana wanahitaji huduma muafaka ya afya na kwanini ni wajibu wetu kuhakikisha wanakuwa na afya bora ya kiwango cha juu"