Skip to main content

Ugonjwa wa Fistula na juhudi za kuukabili nchini Uganda

Ugonjwa wa Fistula na juhudi za kuukabili nchini Uganda

Zikiwa zimesalia siku chake dunia iadhimishe siku ya Kimataifa ya fistula mwaka huu Mei 23, mbiu ya kuutokomeza ugonjwa huu unaowakumba wanawake na wasichana kutokana na kuchelewa kupata huduma stahiki wakati wa kujifungua inapigwa na wadau mbalimbali.

Kiranja katika harakati hizi ni shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA, ambalo linasema juhudi zinahitajika ili kupeleka huduma za afya ya uzazi katika jamii duniani kote, kwani bado visa 50,000 hadi 100,000 vya fistula hubainika kila mwaka.

Takribani wanawake milioni mbili wanaishi na Fistula, wakiugulia maumivu makali, hukumbana na unyanyapaa katika jamii nyingi hususani barani Afrika. Hali hiyo imesababisha wengi wao kuishi katika ubaguzi na maisha ya kutengwa.

Kufahamu hali ilivyo Afrika Mashariki nchini Uganda tuungane na mwandishi wetu John Kibego aliyefualitia hali ya mwanamke aliyetengwa kabisa katika jamii na kulazimika kutembea kilomita tisini alipopashwa taarifa za kuwepo kwa matibabu ya bure baada ya kuishi karibu muongo moja na fistula.

 (MAKALA KIBEGO)