Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO na Muungano wa Ulaya kupambana na ukataji haramu wa miti

FAO na Muungano wa Ulaya kupambana na ukataji haramu wa miti

Muungano wa Ulaya na Shirika la Chakula na kilimo FAO zimeungana kupambana na ukataji haramu wa miti kwenye nchi za kitropiki.

Taarifa iliyotolewa na FAO imeeleza kwamba lengo ni kupunguza madhara kwa mazingira na pia kuimarisha vipato vya jamii zinazotegemea misitu kuishi.

Kwa mujibu wa FAO, ukataji haramu wa miti unagharimu serikali zaidi ya dola bilioni 10 kwa mwaka.

Muungano wa Ulaya na nchi zingine za Ulaya zimetoa ufadhili wa dola milioni 30 kwa ajili ya mradi huo.

Robert Simpson ni mkurugenzi wa mpango wa sheria na utawala wa misitu wa FAO.

(Sauti ya Bwana Simpson)

“Mradi unawapatia wadau usaidizi wa taaluma na fedha kupitia miradi na mazungumzo na serikali. Tunasaidia mashirika ya sekta binafsi, taasisi za serikali na jamii ili kukabiliana na changamoto zilizobainiwa za utawala wa msitu.”