Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wa Ethiopia wanapata msaada baada ya muafaka wa kuachiliwa:UNICEF

Watoto wa Ethiopia wanapata msaada baada ya muafaka wa kuachiliwa:UNICEF

Nchini Ethiopia msaada unatolewa kwa watoto waliotekwa wakati wa wizi wa ng’ombe Mashariki mwa nchi hiyo , na baadaye kuachiliwa, umesema leo Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF , watoto 10 wameachiwa huru Jumatano wiki hii na wengine 19 waliachiwa wiki iliyopita.

Jumla ya watoto 146 walitekwa wakati wa shambulio ambalo makundi ya Sudan Kusini yameshutumiwa kufanya na kulenga jimbo la Gambella.

Msemaji wa UNICEF ni Christophe Boulierac:

(SAUTI YA BOULIERAC)

Lazima mjue kwamba wizi wa ng’ombe sio kitu kipya, lakini kipya ni kwamba umeendelea kuwa hatari .Awali hawakuwa wanahusisha mauaji, lakini sasa wanafanya hivyo na wanawateka watoto”

UNICEF inasema watoto hao walioachiliwa wana umri kati ya miezi mine na miaka tisa. Baadhi yao wana utapia mlo wa kupindukia na wanapatiwa matibabu pamoja na kupewa ushauri nasaha.