Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamishna wa UNRWA azuru Syria, akutana na wakimbizi

Kamishna wa UNRWA azuru Syria, akutana na wakimbizi

Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina-UNRWA Pierre Krähenbühl ametembelea Syria na kukutana na wafanyakazi na maafisa wa serikali.

Akiwa ziarani nchini humo Kamishna Krähenbühl amezungumza na wakimbizi na kusilikiliza madhila na ukatili wanaokutana nao mathalani wakimbizi wa Palestina walionusurika kufuatia shambulio la bomu katika gari mnamo Februari 21 ambao walieleza mstuko alioupata.

‘‘Katika macho Rana na Isara nimeona kisichoelezeka lakini pia matarajio yao ya kusonga mbele’’ alisema Kamishna Krähenbühl baada ya kusikiliza ushuhuda wa manusura."

Kadhalika kiongozi huyo amekutana na wakimbizi wa Palestina walioko Yarmouk na kushuhudia zoezi la ugawaji wa chakula na vifaa vya kujisafi pamoja na huduma za afya zinazotolewa na UNRWA.