Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zeid akubali mwaliko wa Uturuki kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu

Zeid akubali mwaliko wa Uturuki kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu

Uturuki imetoa mwaliko kwa Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein kuzuru taifa hilo kufuatia hofu iliyotokana na taarifa za kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu .

Ofisi ya Kamishina mkuu imesema mwaliko umepokelewa lakini haujaenda mbali zaidi. Ofimeongeza kuwa wanachotaka ni fursa isiyo na pingamizi kwa wataalamu wa haki za binadamu kuweza kuwafikia watu katika maeneo ya kusini Mashariki mwa nchi, lakini sio zoezi la uhusiano wa umma.

Ukiukwaji huo unajumuisha taarifa za wanawake na watoto wasio na silaha zozote kushambuliwa na walenga shabaha, lakini pia magari ya kubeba wagonjwa kuzuiliwa na pande zote katika mgogoro kuwafikia majeruhi.

Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu...

(SAUTI YA COLVILLE)

“Kama tulivyosema tunataka fursa kuwafikia watu wenyewe Chizre. Na maeneo mengine ambako kumeripotiwa mapigano na ukiukwaji , tunachosema ni kwamba kuna taarifa za mbaya na kamishina mwenyewe kwenda huko haitasaidia , anachokitaka ni ziara ya kina ya wataalamu wenye uzoefu , na siozoezi la uhusiano wa umma”