Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi na wahamiaji 1000 waokolewa pwani ya Italia:UNHCR

Wakimbizi na wahamiaji 1000 waokolewa pwani ya Italia:UNHCR

Takribani watu 1000 wa mataifa mbalimbali zikiwemo familia za wakimbizi, wahamiaji  na watoto walio peke yao wameokolewa katika pwani ya Italia.Flora Nducha na taarifa zaidi

(TAARIFA YA FLORA)

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR , watu wapatao 500 waliokuwa wanasafiri kutumia boti mbili za uvuvi zilizoondoka siku kadhaa zilizopita nchini Misri wameokolewa kwenye mwambao wa Sicily, Kusini Mashariki mwa Cape Passero, wakiwemo watu kutoka Iraq na Syria.

Mbali ya boti hizo mbili kumekuwepo na boti nyingine kutoka Libya ambayo ilikuwa na watu wengi na 1000 waliookolewa jana wanasafirishwa leo na kupelekwa maeneo manne tofauti Italia ya Catania, Palermo, Augusta na Crotone, William Spindler ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA SPINDLER)

"UNHCR inaendelea kupigia chepuo uwepo wa njia sahihi za kisheria kusafiri Ulaya kwa kuwapa makazi na kupitia programu za kibinadamu, kuunganishwa kwa familia, mwaliko binafsi au kupitia visa za wanafunzi au kazi na kadhalika kama mbinu ya kusitisha usafirishaji haramu wa binadamu."