Skip to main content

Nchini DRC, watu wa asili waendelea kunyanyaswa

Nchini DRC, watu wa asili waendelea kunyanyaswa

Haki za watu wa jamii za asili bado hazitambuliwi ipasavyo, amesema mmoja wa wawakilishi wanaohudhuria mkutano wa 15 wa mjadala wa kudumu wa watu wa asili unaofanyika mjini New York Marekani.

Mochire Diel ni mwakilishi wa watu wa jamii ya Bambuti nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ambao kwa mujibu wake idadi yao nchini humo ni takriban 750,000.

Amezungumzia uhalifu uliofanyika dhidi ya jamii hii wakati wa vita vilivyoathiri mashariki mwa nchi hii, ambao umethibitishwa pia na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu kwenye ripoti zake maalum za 2010 na 2014.

Kwenye mahojiano na Priscilla Lecomte wa idhaa hii Mochiré Diel anaeleza jinsi jamii hii inavyozidi kunyanyaswa.