Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa ukanda wa mashariki na Afrika kaskazini wajadili uhakika wa chakula:FAO

Mkutano wa ukanda wa mashariki na Afrika kaskazini wajadili uhakika wa chakula:FAO

Mkutano wa kikanda kwa ajili ya mataifa ya Mashariki na Afrika ya Kaskazini unafanyika Roma Italia kujadili vipaumbele vya uhakika wa chakula.

Mkutano huu umewaleta pamoja mawaziri wa kilimo, maafisa wa ngazi za juu , wawakilishi kutoka asasi za kiraia na sekta binafsi ambao wanajikita kutoka na mpango maalumu wataoutumia siku za usoni kwa pamoja kukabiliana na changamoto za uhakika wa chakula.

Miongoni mwa changamoto hizo ni zile zinazohusiana na kilimo , lishe na maendeleo vijijini katika kanda ya Mashariki na Afrika ya Kaskazini, na kutanabahi kutoka kwa yale waliojifunza katika miaka ya karibuni ambayo yataweza kutumika kuunda mkakati wa pamoja kukabiliana na matatizo yanayowasibu wote.

Washiriki takribani 150 wanahudhuria mkutano huo utakaomalizika kesho Ijumaa.