Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchafuzi wa hewa waongezeka duniani: WHO

Uchafuzi wa hewa waongezeka duniani: WHO

Asilimia 98 ya miji mikubwa yenye zaidi ya wakazi 100,000 duniani kote haina hewa safi ya kupumua, limesema shirika la Afya Duniani WHO katika ripoti yake..

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa leo, uchafuzi wa hewa unazidi kuongezeka duniani kote, na kusababisha zaidi ya vifo milioni tatu kila mwaka, kupitia maradhi ya kiharusi, mshtuko wa moyo, pumu, saratani na magonjwa mengine.

Miji iliyoathirika zaidi na tatizo hilo na ile iliyo kwenye nchi za kipato cha chini au cha kati.

Maria Neira ni mkurugenzi wa idara ya afya ya umma ya WHO.

(Sauti ya Bi Maria)

Kwa ujumla, asilimia 80 ya idadi ya watu wanaoishi mijini ambapo ubora wa hewa unafuatiliwa wamekumbwa na viwango vya uchafuzi vinavyozidi vile vilivyopendekezwa na WHO, na wakati mwingine mara kumi zaidi ya viwango vilivyopendekezwa na WHO.”

Ripoti hiyo imekusanya takwimu kutoka miji 3,000 kwenye nchi 103, WHO ikifuraishwa kuona kwamba nchi nyingi zaidi hujali kiwango cha uchafuzi wa hewa.