Skip to main content

Ushirika imara wahitajika katika ujenzi wa amani-Afrika

Ushirika imara wahitajika katika ujenzi wa amani-Afrika

Wito umetolewa wa ushirika imara katika ujenzi wa amani kati ya Umoja wa mataifa na mashirika ya kikanda ya Afrika. Taarifa zaidi na Flora Nducha.

(TAARIFA YA FLORA)

Wito huo umetolewa leo kwenye mjadala maalumu kuhusu kudumisha amani:mkakati, ushirika na mustakhbali wa ujenzi wa Amani Afrika unachofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York ukijumuisha Ofisi ya Umoja wa mataifa ya mshauri maalumu kuhusu masuala ya Afrika,OSAA, ofisi ya uungaji mkono masuiala ya ujenzi wa amani na Muungano wa Afrika.

Mkutano unalenga kuendeleza kasi ya kisiasa kwa ujenzi wa amani barani Afrika na kujadili njia za kutekeleza mapendekezo na maelekezo ya tathmini ya Umoja wa Mataifa ya uimarishaji amani yaliyopitishwa tarehe 27 Aprili 2015.

Akizungumza katika mjadala mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Macharia Kamau ambaye pia ni mwenyekitu wa tume ya Umoja wa Mataifa ya ujenzi wa amani amesema

(MACHARIA KAMAU)

"Ni lazima tukubali kwamba bila ya amani hakutakuwa na maendeleo na Afrika inahitaji sanan maendeleo kuondokana na hali ya sasa. Lakini ni lazima tukubali kwamba Afrika imepiga hatua katika ujenzi wa amani, Afrika ya miaka ya 70,80, na 90 siyo afrika ya sasa na tusipokiri mafanikio hayo basi hatuwezi kusonga mbele zaidi na amani."