Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upimaji kasi na tiba nafuu yaleta matumaini kwa wagonjwa wa TB

Upimaji kasi na tiba nafuu yaleta matumaini kwa wagonjwa wa TB

Shirika la Afya Duniani (WHO), limetoa mapendekezo mapya yanayolenga kuongeza kasi ya kugundua na kuboresha matibabu dhidi ya kifua kikuu sugu (MDR-TB), kwa kutumia njia mpya ya kupima haraka na kuutibu ugonjwa huo kwa kipindi kifupi zaidi, na kwa gharama nafuu. Grace Kaneiya na taarifa kamili.

(TAARIFA YA GRACE)

Mkurugenzi wa WHO kuhusu matibabu ya TB duniani, Dkt. Mario Raviglione, amesema njia hiyo mpya ni hatua muhimu katika kukabiliana na TB sugu kama tatizo la afya ya umma.

Amesema mapendekezo hayo mapya ya WHO yanatoa matumaini kwa mamia ya maelfu ya wagonjwa wa MDR-TB, ambao sasa wanaweza kunufaika kwa upimaji unaoweza kutambua ni nani anafaa kupewa tiba ya muda mfupi, na hivyo kuweza kumaliza matibabu kwa nusu ya kipindi na gharama ya matibabu ya awali.

(SAUTI DK MARIO RAVIGLIONE)

"Uchunguzi huu wa haraka na matibabu rahisi ,hakika unaweza kusaidia kukabiliana na kifua kikuu kwakuwa twapaswa kukabIliana na kifua kikuu kote dunaiani kwani ni janga."

Kwa gharama ya chini ya dola 1,000 za Kimarekani kwa kila mgonjwa, tiba mpya ya TB sugu inaweza kukamilishwa kwa kipindi cha miezi tisa hadi kumi na miwili, na hivyo kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na TB.