Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauritania iko katika hatari ya kuyumba isipogawana utajiri sawia

Mauritania iko katika hatari ya kuyumba isipogawana utajiri sawia

Mwakilishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ufukara wa kupindukia na haki za binadamu Philip Alston, leo amesema utulivu ulioshamiri Mauritania uko hatarini endpo matunda ya maendeleo hayotugawanywa sawia na kunufaisha wote.

Ameongeza kuwa serikali ya Mauritania inahitaji kuongeza juhudi katika kutekeleza ahadi zake za kukomesha kasumba za utumwa, na kusonga mbele zaidi ya mtazamo wa uhisani, na kuwa na mtazamo unaotambua ambao unatambua kwamba kila Mmauritania ana haki ya maji, huduma za afya, elimu na chakula.

Bwana Alston ameyasema hayo akihitimisha ziara yake ya kwanza nchini humo.

Amelielezea taifa la Mauritania kama lenye utajiri wa maliasili , na lenye mtazamo ambao haukubali tena utumwa , limedumisha utulivu na kufurahia kiwango kikubwa cha misaada ya kimataifa ya maendeleo.

Amesema anatumbu hatua kubwa iliyopigwa na taifa hilo lakini akaonya kwamba asilimia 44 ya watu wa vijijini wanaishi katika ufukara wa kupindukia hasa katika mikoa ya Gorgol, Brakna, na Trarza aliyoitembelea.