Skip to main content

Mkutano wa Istanbul ni fursa ya kutoa misaada ya kibinadamu:O'Brien

Mkutano wa Istanbul ni fursa ya kutoa misaada ya kibinadamu:O'Brien

Mkutano kuhusu misaada ya kibinadamu unaotarajiwa kuanza Mei 24 nchini Uturuki ni fursa muhimu kwa ajili ya kusaidia waathirika wa majanga ya asili na kibinadamu ikiwamo vita na mabadiliko ya tabianchi.

Akihojiwa na redio ya Umoja wa Mataifa mjini New York Mratibu Mkuu wa Masuala ya Kibinadamu katika Umoja wa Mataifa Stephen O'Brien amesema mkutano huo utakaokutanisha jumuiya ya kimataifa unatoa mwanya wa kuchangia fedha na kujali makundi ya wanaoteseka katika majanga.

Akitolea mfano amesema hivi karibuni alikutana na wakimbizi wa Syria waishio nchini Jordan na kumhoji mmoja wao anachotaka.

( SAUTI ya OBRIEN)

‘‘Alinitizama kama anayesema kwanini kuniuliza swali kama hilo?. Ni wazi kwamba nataka kurudi nyumbani. Kulikokuwa nyumbani kwako ndiko unakoweza kurudi na kujenga upya maisha yako, na kuipa familia yako ulinzi na uhakika wa mustakabali’’

Amesisitiza kwamba misaada ya kibinadamu sio jukumu la Umoja wa Mataifa pekee, akizitaka nchi na mashirika kujikita katika kusaidia jamii zilizoathirika.