Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa PBF ni mfano wa chanda chema huvikwa pete - Kenya

Mradi wa PBF ni mfano wa chanda chema huvikwa pete - Kenya

Kujifungua kijijini nchini Kenya ina hatari zake na maelfu ya akina mama hufariki kila mwaka kutokana na matatizo wakati wa kujifungua.

Kwa sasa wanawake wanajifungua katika vituo vya afya kufuatia mpango wa ubunifu (PBF) ambao unalenga kuwatunuku akina mama na watoa huduma za afya. Matokeo yake ni huduma bora kwa mama na watoto kabla na baada ya kuzaliwa.

Mradi kama huu ni mpango ambao unafadhiliwa na serikali husika na wadau na unalenga uwekezaji ambao unazaa matunda. Basi ungana na Grace Kaneiya katika makala hii.