Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Somalia inahitaji msaada wa haraka baada ya kukumbwa na ukame:OCHA

Somalia inahitaji msaada wa haraka baada ya kukumbwa na ukame:OCHA

Zaidi ya watu milioni 1 nchini Somalia wako katika hatari kuangukia kwenye ukosefu wa uhakika wa chakula endapo hawatopata msaada umeonya Umoja wa Umoja wa mataifa hii leo. Ukame uliokithiri kwenye majimbo yaliyojitenga ya Puntland na Somaliland tayari umeshasababisha athari kubwa kwenye jamii hizo ambapo watu 385,000 hawana uhakika wa chakula.

Katika maeneo mengine asilimia 60 hadi 80 ya mifungo imeangamia kwa njaa. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kutratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA , asilimia 37 ya watu wote katika majimbo hayo wanahitaji aina Fulani ya msaada wa kibinadamu.

Peter de Clercq,mratibu wa masuala ya kibinadamu Somalia amependekeza kutoa chanjo kwa mifugo na kuwapa msaada wa fedha wakulina na wafugaji ili kukabiliana na athari za ukame.