Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Biashara ya quinoa yanufaisha jamii za vijijini Peru

Biashara ya quinoa yanufaisha jamii za vijijini Peru

Utafiti mpya wa Kituo cha Kimataifa cha Biashara (ITC) umebaini kuwa ununuaji wa zao la quinoa unachangia kuboresha maisha ya jamii za vijijini, hususan wanawake nchini Peru.

Utafiti huo umeonyesha kwamba kuongezeka kwa watu wanaolitumia zao la quinoa kama chakula Marekani na Ulaya kati ya mwaka 2013 na 2014, kulichangia kupanda kwa bei ya zao hilo lenye asili ya kanda ya Andean, Amerika ya Kusini, na hivyo kuwanufaisha wakulima wadogowadogo na jamii za vijijini nchini Peru.

Kwa upande mwingine, utafiti huo wa mwaka mzima uliofanyika kati ya 2014 na 2015, ukijumuisha kaya 150 nchini Peru, umeonyesha kuwa kushuka kwa bei ya quinoa mnamo 2014, kulichangia jamii hizo za vijijini kuwa na kipato kidogo, n ahata kupunguza kiasi cha chakula kinachotumiwa na kila kaya.