Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO na washindi wa Nobel waangalia uhakika wa chakula unavyohusiana na amani

FAO na washindi wa Nobel waangalia uhakika wa chakula unavyohusiana na amani

Washindi wanne wa tuzo ya Nobel wamejiunga kwenye juhudi za Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) za kukabiliana na njaa na machafuko. Taarifa kamili na Priscilla Lecomte

(Taarifa ya Priscilla)

Washindi hao wa tuzo ya Nobel ni Muhammad Yunus aliyetuzwa mwaka 2006 kwa kutoa mikopo ya fedha kwa watu maskini, Oscar Arias Sánchez aliyepokea tuzo yake mwaka 1987 kwa juhudi zake katika kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe Amerika ya Kati, Tawakkol Karman aliyetuzwa mwaka 2011 kwa kupigania amani na haki za wanawake nchini Yemen, na mwanaharakati wa amani, Betty Williams kutoka Ireland, aliyepewa tuzo hiyo mwaka 1976.

Wanne hao wamekaribishwa jijini Roma Italia kushiriki hafla ya kuzindua mchakato mpya wa FAO na Washindi wa Tuzo ya Nobel kuhusu uhakika wa kupata chakula na amani, ambapo watatoa ushauri kwa FAO kuhusu jinsi ya kuimarisha uhusiano kati ya amani na uhakika wa chakula katika nchi mbalimbali.