Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lajadili itikadi kali

Baraza la usalama lajadili itikadi kali

Kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo kumefanyika mjadala kuhusu jinsi ya kupambana na itikadi za vikundi vya kigaidi. Taarifa zaidi na Flora Nducha.

(Taarifa ya Flora)

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na Mwakilishi wa Kudumu wa Misri kwenye Umoja wa Mataifa, itikadi hizo huwezesha vikundi kama ISIS kuhalalisha mauaji ya raia na kuajiri maelfu ya vijana duniani kote. ISIS husambaza ujumbe wake kupitia mitandao ya kijamii, ikituma zaidi ya ujumbe 90,000 kila siku kwenye mtandao wa twitter kwa lugha tofauti zaidi ya ishrini.

Akihutubia mjadala huo, Naibu Katibu Mkuu Jan Eliasson amesema ni lazima kuunda mkakati wa kimataifa wa kupambana na itikadi hizo, ambao hautatumia nguvu za kijeshi tu, kwani…

(Sauti ya Bwana Eliasson)

“Tunapaswa kujua kwamba mabomu ya magaidi yanalenga zaidi ya maisha ya binadamu. Yanalenga maadili yetu ya pamoja, na kusambaza hofu. Tunawajibika kulinda watu dhidi ya hatari na hofu hizo na kutunza maadili ya kimataifa.”

Bwana Eliasson amesisitiza umuhimu wa kushirikisha vijana katika juhudi za kuunda suluhu na itikadi mbadala.