Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azindua ripoti ya UM ya gharama za njaa Madagascar

Ban azindua ripoti ya UM ya gharama za njaa Madagascar

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo Jumatano amezindua rasmi ripoti ya Umoja wa mataifa kuhusu gharama za njaa nchini Madagascar.

Ripoti hiyo imezinduliwa wakati akihutubia bunge na seneti mjini Antananarivo na kushukuru mtandao wa wanawake wabunge kwa kuwa kinara kwenye kampeni ya lishe.

Amesema ripoti inatoa taswira ya kutisha , kwani karibu mtoto mmoja kati ya wawili Madagascar wameathirika na matatizo ya kudumaa kutokana na lishe duni.

Ameipongeza serikali kwa juhudi za kuimarisha lishe lakini akaiasa kuwa lishe ni zaidi ya kuwalisha chakula watu, inahitaku kutoa kipaumbele pia katika afaya, kilimo, elimu , kuwawezesha wanawake na suala la maji.

Ameongeza kuwa lishe duni ni zahma kwa watu na janga kwa maendeleo ya taifa kwani inaigharimu Madagascar zaidi ya dola bilioni moja na nusu kila mwaka.