Skip to main content

Kijana ajitolea kwa ajili ya mustakhabali wa watoto wa DRC

Kijana ajitolea kwa ajili ya mustakhabali wa watoto wa DRC

Kwa kipindi cha miaka 15 iliyopita, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC imepiga hatua kubwa katika kuhakikisha watoto wote wanapewa chanjo dhidi ya magonjwa hatari kama vile dondakoo, kifaduro, pepopunda, polio, na surua.

Hata hivyo, bado ni theluthi mbili tu ya watoto nchini kote wamepata chanjo zao zote muhimu.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) linashirikiana na serikali ya DRC katika kutoa chanjo za surua na polio, na dawa ya vitamini A kwa watoto katika majimbo ya mashariki mwa nchi.

Shughuli hizo hutekelezwa kupitia wafanyakazi wa kujitolea wanaotoa chanjo pamoja na kuhamasisha jamii.

Job Ngandu ni mmoja wao. Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii inayoeleza kazi zake.