Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takribani ndege milioni 25 huuawa kila mwaka

Takribani ndege milioni 25 huuawa kila mwaka

Kikozi kazi kipya maalumu kimeundwa Mediterranean ili kukomesha mauaji haramu, kuwachukua na kuwauza ndege wanaohama.

Kikozi kazi hicho kimetangazwa leo na mkataba kuhusu viumbe vinavyohama (CMS) katika siku maalumu ya kimataifa ya kuhama kwa ndege na kinahusisha mataifa mbalimbali na muungano wa tume ya Ulaya.

Washirika wengine katika muungano huo ni shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa mazingira UNEP, ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC,mikataba ya kimataifa ya mazingira, INTERPOL, vyombo vya dola, jamii za wawindaji na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Kauli mbiu mwaka huu ni “wakati anga imenyamaa kimya , acha uuaji haramu, kuwachukua na biashara ya ndege” Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la BirdLife inakadiriwa kuwa ndenge milioni 25 zikiwemo aina zilizo hatarini kutoweka huuawa kila mwaka kwenye bahari ya Mediterranean