Skip to main content

Zeid asikitishwa na ukatili dhidi ya raia Uturuki

Zeid asikitishwa na ukatili dhidi ya raia Uturuki

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein, amesema amepokea taarifa za ukatili unaodaiwa kufanywa na vikosi vyajeshi na usalama vya Uturuki katika miezi kadhaa iliyopita na kuzitaka mamlaka za nchi hiyo kuruhusu uchunguzi huru.

Akiongea mjini Geneva hii leo Kamishina Zeid amesema Uturuki inapaswa kuruhusu wachunguzi huru wakiwamo wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kufika Kusini Mashariki mwa eneo hilo kufanya uchunguzi wa wazi na huru dhidi ya tuhuma hizo.

Amelaani ukatili na vitendo vingine kinyume na sheria vinavyotekelezwa na vikundi vya vijana na vikundi visivyo vya kiserikali huko Cizre na maeneo mengine na kuelezea kusikitishwa kwake kufuatia vifo vitokanavyo na vitendo vya kigaidi.