Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi mpya wa UNICEF wapambana na unyanyasaji wa watoto mitandaoni

Mradi mpya wa UNICEF wapambana na unyanyasaji wa watoto mitandaoni

Nyenzo mpya ya kusambaza taarifa na takwimu kuhusu uhalifu dhidi ya watoto kwenye Intanet imezinduliwa leo kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Taarifa ya UNICEF imeeleza kwamba nyenzo hiyo mpya itachangia kupambana na unyanyasaji wa kijinsia unaofanyika kupitia mtandao wa Intaneti.

UNICEF imeongeza kwamba kadri upatikanaji wa huduma za intanet na simu za mkononi unavyozidi kuenea duniani kote, watoto wanazidi kupata fursa zaidi za elimu lakini vile vile kuwa hatarini kunyanyaswa mitandaoni.

Tovuti hiyo iitwayo GRID inawezesha serikali, walimu na polisi kupata takwimu na mifano ya njia bora za kupambana na unyanyasaji huo.