Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatari ya tsunami bahari ya Hindi yajadiliwa kwenye mkutano wa kimataifa

Hatari ya tsunami bahari ya Hindi yajadiliwa kwenye mkutano wa kimataifa

Wataalamu wa Tsunami kutoka ukanda wa bahari ya Hindi wanakutana Australia wiki hii kusaka njia za kuimarisha uwezo wa kuzuia zahma kama ya mwaka 2004 katika ukanda huo.

Mkutano huo wa siku tano unaendeshwa na tume ya serikali za kimataifa ya masuala ya bahatri katika shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO (IOC) na mwenyeji kitengo cha utabiri wa hali ya hewa cha Australia.

Mkutano huo umeanza kwa kuzungumzia mfululizo wa matukio duniani kote ikiwa kama matayarisho ya maadhimisho ya kwanza ya siku ya kimataifa ya elimu kuhusu tsunami yatakayofanyika Novemba 5. Akizungumza katika mkutano huo naibu mkurugenzi na mkuu wa kitengo cha madhara, onyo na utabiri katika idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini humo bwana Rob Webb amesema ukiangalia historia tsunami haijali mipaka hivyo ni muhimu sana kulitafakari tatizo hilo kimataifa na kuchukua hatua za kimataifa.

Mbali ya kuangalia peopngo lililopo katika utoaji tahadahari na mfumo wa mawasiliano, mkutano huo unaangalia jinsi ya kuboresha wigo wa kunakofika taarifa ili watu waweze kujiandaa na kuchukua hatua mapema, kuokoa maisha yao na mali zao. Wajumbe kutoka mataifa 14 wanahudhuria mkutano huo.