Skip to main content

Twatumai serikali itatangua tangazo la kufunga kambi-Kenya: UNHCR

Twatumai serikali itatangua tangazo la kufunga kambi-Kenya: UNHCR

Wakati serikali ya Kenya imetangaza hatua ya kufunga kambi nchini Kenya, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limesema kwamba litaendelea kufanya kazi na serikali ili kuhakikisha kwamba takriban wakimbizi 600,000 hawataathirika.

Katika mahojiano maalum na Grace Kaneiya wa Idhaa hii, Duke Mwancha, Kaimu msemaji wa UNHCR nchini Kenya amesema kwamba mazungumzo yanaendelea na serikali ya Kenya. Kwanza anaanza kwa kueleza tamko lao baada ya taarifa ya serikali ya Ijumaa Mei 6.