Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bugando yahitaji Euro Milioni 200 kukamilisha kituo cha tiba dhidi ya saratani

Bugando yahitaji Euro Milioni 200 kukamilisha kituo cha tiba dhidi ya saratani

Nchini Tanzania kitengo cha matibabu dhidi ya saratani katika hospitali ya rufaa ya Bugando, mkoani Mwanza kilianza huduma mwaka 2009. Hadi sasa kila mwaka wagonjwa wapatao 3500 husaka huduma huku asilimia 50 kati yao wakihitaji huduma za mionzi.

Serikali ya Tanzania imeweka shime na kuimarisha mahitaji muhimu lakini bado kuna changamoto ambazo ziliwekwa bayana wakati wa ziara ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kama anavyoelezea Assumpta Massoi kwenye makala hii iliyowezeshwa na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini humo.