Skip to main content

Ili kutimiza malengo ya SDG’s mtazamo lazima ubadilike:Ban

Ili kutimiza malengo ya SDG’s mtazamo lazima ubadilike:Ban

Ili kutimiza ajenda na maendeleo endelevu ya 2030 mtazamo ni lazima ubadilike, kuwe na utashi wa kisiasa, mshikamano wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo na kuona mbali zaidi ya kasumba zilizozoeleka. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwenye tukio maalumu kuhusu maendeleo endelevu nchini Mauritius.Taarifa kamili na John Kibego..

(Taarifa ya Kibego)

Amesema ajenda yam mwaka 2030 inahitaji mpiango sera, au hatua zozote ziwafikirie watu wasiojiweza, kuto kipaumbele kwa masuala ya muhimu ikiwemo uchumi na maendeleo na ni jukumu la kila nchi na kila mtu. Na akalipongeza taifa la Mauritius kwa kulitambua hilo..

(SAUTI YA BAN)

“Lakini ajenda hii haiwezi kutimizwa New York au Geneva. Itatokea katika jamii na itamuhitaji kila mtu. Ndio sababu nimetiwa moyo na jitihada zenu leo.Mnajua ni lazima tuwahusishe viongozi kama mlio nao hapa kwenye asasi za kiraia, ni nyie mtakaosaidia kuunda na kutekeleza sera na kuwawajibisha viongozi”