Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuendelea kukandamiza waandamanaji ni kikwazo kwa haki za binadamu Misri

Kuendelea kukandamiza waandamanaji ni kikwazo kwa haki za binadamu Misri

Wataalamu watatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu leo Jumatatu wameitaka serikali ya Misri kukomesha hatua inazochukua dhidi ya wanaotekeleza haki zao za kukusanyika n kujieleza nchini humo.

Wataalamu hao ambao ni Mwakilishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Uhuru wa Kujieleza David Kaye, Uhuru wa Kukusanyika kwa Aamani na Kuchangamana Maina Kiai na yule wa Watetezi wa Haki za Binadamu Michel Forst , wamesena ongezeko la kuwakandamiza zaidi watu wanaoandamana kwa amani nchini Misri ni kikwazo katika kufungua mlango wa mazingira mazuri ya kisiasa na kijamii nchini humo.

Wameongeza kuwa matumizi ya nguvu dhidi ya asasi za kiraia na wanaotoa maoni yao ya kisiasa , vinachangia kuzorotesha mazingira ya kuchagiza na kulinda haki za msingi ambazo ni chachu ya kuwa na jamii ya kidemokrasia.

Wamelaanihatua kali zinazochukuliwa na serikali kwa miama miwili iliyopita dhidi ya waandamanaji, waandishi wa habari, watetezi wa haki za binadamu na wanasheria na kuitaka nchi hiyo kusitisha mara moja hatua hizo.