Kobler alaani vikali shambulio dhidi ya waandamanaji Benghazi

8 Mei 2016

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu na mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa Libya (UNSMIL) Martin Kobler amelaani vikali shambilio dhidi ya waandamanaji kwenye uwanja wa al-Kish Square mjini Benghazi Libya lililotokea mchana wa Mai 6.

Kwa mujibu wa taarifa ya UNSMIL, watu wane akiwemo mwanamke na mtoto wa miaka 12 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Duru zinasema makombora kadhaa au magruneti yalianguka kwenye uwanja huo wakati ambapo umati wa watu walikuwa wanaandamana.

Bwana Kobler amesema amesikitishwa saana na shambulo hilo dhidi ya watu waliokuwa wakiandamana kwa Amani na ametuma salamu za rambirambi kwa familia za marehemu na kuwatakia afueni ya haraka majeruhi.

Ametoa wito wa kuhakikisha yeyote aliyehusika na ukatili huo kuwajibisha akiongeza kuwa ni kinyume na sharia za binadamu za kimataifa kushambulia raia na huo ni uhalifu wa vita, na wahusika wachukuliwe hatua za kisheria ikiwemo katika Mahakam ya kimataifa ya uhalifu ICC ambayo ina mamlaka ya kufanya hivyo kwa Libya.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter