Skip to main content

UNAMA yasikitishwa na hukumu ya kifo iliyotekelezwa leo Afghanistan:

UNAMA yasikitishwa na hukumu ya kifo iliyotekelezwa leo Afghanistan:

Licha ya wito unaoendelea kutolewa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya utekelezaji wa hukumu ya kifo, mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA unasikitika kufuatia kunyongwa kwa watu sita mapema leo , wanaodaiwa kutekeleza uhalifu mkubwa ukiwemo dhidi ya raia.

Umoja wa Mataifa unabainisha kwamba hakuna ushahidi wa thamani ya kutumia hukumu ya kifo na kwamba matumizi ya adhabu ya kifo hayachangii usalama wa umma.

UNAMA unaichagiza serikali ya Afghanistan kufanya haraka mabadiliko ya mfumo wa sheria ambayo yataruhusu hukumu za kifo kubadilishwa na kuwa vifungo vya maisha.