Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na dunia hakikisheni SIDS hayangamii kabisa:Sonam Tsultrim

UM na dunia hakikisheni SIDS hayangamii kabisa:Sonam Tsultrim

Dunia inahitaji kuheshimu na kutekeleza maamuzi ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa.

Wito huo umo katika barua maalumu ilisomwa nab inti wa mika 15 Sonam Tsultrim mbele ya katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon nchini Ushelishel.

Binti huyo wa senkodari amewito kwa dunia kwa niaba ya watu wa mataifa ya visiwa vidogo vinavyoendelea SIDS, ili kuili kuokoa visiwa hivyo ili visiendelee kuzama Zaidi.

Akisoma barua hiyo kwa unyeyekevu na hisia kali biti huyo amesema wito huo unagusa mataifa yote sio tuu mataifa madogo bali pia mataifa tajiri na yaliyoendelea kwa tatizo la mabadiliko ya tabia nchi linakumba mataifa yote ya SIDS yako katika hatari kubwa.

image
Mtoto Sonam Tsultrim akisalimiana na Ban Ki-moon baada ya kusoma barua:Picha na UN/Newton Kanhema
Akamgeukia Katibu Mkuu Ban na kufunguka

(SAUTI YA SONAM TSULTRIM)

“ Kwa hiyo Bwana. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nkusihi kufanya uwezalokwasababu mambo haya ni ya muhimu mkubwa na yanaathiri binadamu wote. Huu si mzaha tena; ni suala la kuwepo taifa letu au kutokomea, ambapo itakuwa hivyo mwishowe kama maombi yetu hayatozingatiwa”