Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wa asili kusaka njia kuzuia mizozo na kuleta amani kuanzia Mai 9-20

Watu wa asili kusaka njia kuzuia mizozo na kuleta amani kuanzia Mai 9-20

Zaidi ya washiriki 1000 kutika jamii mbalimbali za watu wa asili duniani wanatarajiwa kuhudhuria kongamano la 15 la Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya watu wa asili litakaloanza makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York kuanzia Mai 9 hadi 20.

Masuala ya Amani na mizozo, ambayo mara nyingi huzighubika jamii za watu wa asili zikihusiana na mambo ya ardhi, mipaka na rasilimali , pia haki zao na uttaifa wao, yatakuwa miongoni mwa mada zitakazojadiliwa wakati wa kongamano la mwaka huu.

Kwa mujibu wa Alvalo Pop mwenyekiti ajaye wa kongamano hilo , tangu lililpoanzishwa limekuwa likielezea hofu yake dhidi ya mizozo inayoathiri jamii mbalimbali za watu wa asili duniani.

Akisema wanataka kutanabaisha changamoto zinazowakabili watu wa asili katika mizozo na umuhimu wa mchango wa watu wa asili na utamaduni wao katika kuzuia mizozo hiyo na kuleta Amani ya kudumu.

Kongamano hiloo pia litaangalia masuala yanayowagusa vijana wa jamii za watu wa asili, afya, elimu, lugha, haki za binadamu, maendeleo ya kiuchumi na kijamii, mazingira na utamaduni , pia kufualiatia yaliyoafikiwa baada ya kongamano la mwaka 2014.