Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushelisheli yachagizwa kuendelea na uwezeshaji wanawake:Ban

Ushelisheli yachagizwa kuendelea na uwezeshaji wanawake:Ban

Ushelisheli imechagizwa kuendelea na juhudi za kuwezesha wanawake na ushiriki wao mkubwa katika bunge la kisiwa hicho. Hayo yamezungumzwa katika mkutabo baina ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Maita Ban Ki-moon, Rais wa Ushelisheli James A. Michel na baraza la mawaziri la nchi hiyo Jumamosi.

Bana amewahimiza pia viongozi hao kuendelea na jukumu lao katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu yam waka 2030.

Ban pia amewaeleza viongozi hao umuhimu wa kushughulikia mizizi ya ghasia zitokanazo na itikadi kali, lakini pia kuwashirikisha vijana katika ujenzi wa jamii imara.