Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu wa UM awasili Ushelisheli

Katibu Mkuu wa UM awasili Ushelisheli

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewasili kisiwani Ushelisheli Jumamosi . Katika ziara hiyo ya siku mbili Ban atazungumza na Rais Jams.A.Michel, atazuru eneo la hifadhi la Vallee de Mai ambalo ni la urithi wa dunia, atakutana na baraza la mawaziri na kuhutubia bunge.

Kabla ya kuondoka Jumapili , Ban ataruzu kasri linalohusika na masuala ya haki, kituo cha walinzi wa pwani wa shelisheli na kutembelea bustan za mlima Fleuri.

Ban ni Katibu Mkuu wa kwanza wa Umoja wa Mataifa kuzuru Ushelisheli tangu taifa hilo kujiunga na Umoja wa Mataifa Septemba mwaka 1976. Ziara hii ni ya muhimu kwa Kisiwa hicho kwani inaenda sanjari na maadhimisho ya miaka 40 ya uhuru wa taifa hilo lakini pia tangu ilipojiunga uanachama wa Umoja wa Mataifa.

Ban akiondoka Ushelisheli anaelekea Maurtius.