Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban afuatilia kwa karibu hali ya kisiasa Comoro

Ban afuatilia kwa karibu hali ya kisiasa Comoro

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anafuatilia kwa karibu hali ya kisiasa kisiwani Comoro baada ya uamuzi wa karibuni wa mahakama ya katiba wa kuamuru kurejewa kwa sehemu ya uichaguzi wa Rais na gavana wa Anjouan.

Uchaguzi mpya umepangwa kufanyika tarehe 11 Mai 2016. Ban amerejerea msimamo kwamba anaunga mkono juhudi uongozi wa Comoro za kujenga mazingira ya kujiamini na muafaka kwa ajili ya Amani inayojumuisha wote na uchaguzi wa kuaminika.

Ban ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa utashirikiana kwa karibu na Muungano wa Afrika katika suala hili.Ameitaka serikali ya Comoro na wadau wote kwenye mchakato wa uchaguzi kuheshimu sharia na taratibu zilizopo sanjari na itifaki ya uchaguzi ya 15 Machi 2016.