Skip to main content

WHO imeelezea kusikitishwa na vifo vya watoto wachanga Libya

WHO imeelezea kusikitishwa na vifo vya watoto wachanga Libya

Shirika la afya duniani WHO limeelezea kusikitishwa kwake na kutiwa hofu kufuatia vifio 12 vya watoto wachanga kwenye kituo cha afya cha Sabah kitengo cha dharura khuko Kusini mwa Libya.

Vifo hivyo vimesababishwa na maambukizi ya bakteria na ukosefu wa wahudumu wa afya wenye utaalamu ili kutoa huduma inayostahili.

Kwa mujibu wa Dr Jaffar Hussain mwakilishi wa WHO Libya , vifo hivyo vya kusikitisha vimettokea kwa sababu ambazo zinazuilika na ni ishara ya kusambaratika kwa mfumo wa afya Libya.Kituo cha afya cha Sabah ndio kituo pekee kinachotoa huduma ya uzazi na watoto wachanga katika eneo zima la Kusini mwa Libya.

Amesema endapo hatua hazitochukuliwa haraka basi maisha zaidi yataendelea kupotea, hususani miongoni mwa jamii ya wasiojiweza.

WHO imeitaka serikali ya Libya na jumuiya ya kimataifa kusaidia mpango maalumu wa kibinadamu wa afya nchini humo utaokaoruhusu WHO na washirika wake kuokoa maisha . Mpango huo unahitaji dola milioni 50.4 na WHO inahitaji milioni 15.2 kati ya fedha hizo.