IOM imezitaka nchi za Afrika kuridhia na kutekeleza itifaki ya kutembea kwa uhuru

6 Mei 2016

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limezitaka jamii za kiuchumi za kikanda barani Afrika na nchi wanachama kuridhia na kutekeleza taratibu za watu kutembea kwa uhuru katika kanda hizo ili kuhakikisha ajenda ya mwaka 2063 kuhusu muingiliano wa kikanda inatimizwa.

Ajenda ya mwaka 2063 ni mkakati wa Muungano wa Afrika kwa ajili ya mabadiliko ya kiuchumi na kijamii katika bara hilo kwa miaka 50 ijayo.

Akizungumza kwenye kongamano la kikanda la uhamiaji mjini Lusaka Zambia lililomalizika leo, mkurugenzi mkuu wa IOM William Lacy Swing amewaambia wajumbe wa kongamano hilo kwamba uhamiaji kwa binadamu ni kipengele muhimu katika dunia ya utandawazi na kwa serikali za Afrika ni muhimu katika kuleta mabadiliko.

Msemaji wa IOM Joel Millman anafafanua zaidi:

(Sauti ya bwana Millman)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter