Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNODC yahakikishia Nigeria mshikamano inapopigana na ufisadi, ugaidi na uhalifu

UNODC yahakikishia Nigeria mshikamano inapopigana na ufisadi, ugaidi na uhalifu

Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu dawa za kulevya na uhalifu (UNODC), Yury Fedotov, amekutana leo na Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria, na kumhakikishia uungaji mkono wa shirika lake kwa nchi hiyo inapombana na ufisadi, ugaidi na uhalifu.

Hayo yamekuja wakati Bwana Fedotov akihitimisha ziara ya siku tatu nchini Nigeria, ambapo amesema kuwa Nigeria imepitia matatizo mengi yatokanayo na ufisadi, ugaidi, uharamia na uhalifu mwingine, lakini bado inadhamiria kushirikiana na mashirika ya kimataifa mathalan Umoja wa Mataifa na Muungano wa Ulaya katika kukabiliana na matishio hayo.

Amesema dhamira kama hiyo ni wito kwa jamii ya kimataifa kuendelea kuonyesha ari kama hiyo, na kuongeza juhudi zake maradufu katika kuisaidia Nigeria.