Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Karagwe yaimarisha upatikanaji wa huduma za afya kwa walemavu

Karagwe yaimarisha upatikanaji wa huduma za afya kwa walemavu

Kote duniani, watu wenye ulemavu hukumbwa na changamoto zaidi katika kupata huduma za afya, kulingana na gharama na umbali wa huduma hizo, kwa ripoti iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 50 ya watu wenye ulemavu hawana uwezo wa kugharamia huduma za afya duniani kote, huku ikiwa ni asilimia 30 tu ya watu wasiokuwa na ulemavu.

Wilayani Karagwe, nchini Tanzania, duka jipya limezinduliwa likitoa dawa kwa bei nafuu kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum, hiyo ikiwa ni moja ya mikakati ya kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya bora kwa wote, ambalo ni lengo nambari tatu la malengo ya maendeleo endelevu.

Ungana na Anatory Tumaini kutoka Redio Washirika, Karagwe FM, nchini Tanzania ambaye amehudhuria uzinduzi huo.