Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mawese yachangia kupanda kwa bei ya vyakula Aprili:FAO

Mawese yachangia kupanda kwa bei ya vyakula Aprili:FAO

Bei ya kimataifa ya bidhaa muhimu za vyakula imepanda mwezi wa Aprili na kuashiria mfululizo wa tatu wa ongezeko baada ya kushuka.

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la chakula na kilimo FAO mwezi wa Aprili imeongezeka kwa asilimia 0.7 ikilinganishwa na mwezi wa Machi.

Kwa mujibu wa FAO ongezeko hilo haliko sawia kila mahali, na kwa mwezi wa Aprili kwa kiasi kikubwa limechagizwa na bei ya mafuta ya mawese , lakini pia nafaka, huku bei ya sukari ikishuka baada ya kuwa juu mwezi Machi.