Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Changamoto yetu kubwa DRC ni kusimamia uchaguzi- Polisi MONUSCO

Changamoto yetu kubwa DRC ni kusimamia uchaguzi- Polisi MONUSCO

Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC mwishoni mwa mwaka huu, utakuwa ni changamoto kubwa kwa kitengo cha polisi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO.

Hiyo ni kwa mujibu wa Kamishna Awale Abdounasir, Mkuu wa Polisi, MONUSCO akizungumza baada ya kikao cha kujadili majukumu ya kikosi hicho kufuatia azimio jipya la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililoongeza muda wa MONUSCO hadi mwezi Machi mwakani.

(Sauti ya Kamishna Abdounasir)

“Siyo sisi ambao tutasimamia uchaguzi, bali ni polisi wa kitaif, PNC. Lakini tutaangalia ni jinsi gani tutaambatana na PNC katika kusimamia uchaguzi huo kidemokrasia na sheria. Ni changamoto kubwa kwetu lakini tutajipanga kukabiliana nayo.”