Ziarani Nepal, Jan Eliasson asisitizia mshikamano wa jamii wakati wa mizozo

Ziarani Nepal, Jan Eliasson asisitizia mshikamano wa jamii wakati wa mizozo

Nchini Nepal, Naibu Katibu Mkuu Wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson ameshuhudia uharibifu uliosababishwa na matetemeko ya ardhi yaliyoikumba nchi hiyo mwaka mmoja uliopita.

Ziara hiyo ilikuwa ni sehemu ya kampeni ya kuelimisha jamii iitwayo “mpango maalum wa masuala ya kibinadamu” wakati wa kuelekea kongamano la kimataifa kuhusu masuala ya kibinadamu linalotarajiwa kufanyika mwezi huu mjini Istanbul Uturuki.

Bwana Eliasson amemulika umuhimu wa mshikamano wa wadau wote katika kukabiliana na madhara ya mizozo ya kibinadamu duniani kote.

Kulikoni? Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.