Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano la mchango wa dini katika kuzuia uchocheaji ghasia kufanyika Addis Ababa

Kongamano la mchango wa dini katika kuzuia uchocheaji ghasia kufanyika Addis Ababa

Kongamano kuhusu jukumu la watendaji wa kidini kutoka Afrika katika kuzuia uchochezi wa ghasia zinazoweza kusababisha uhalifu wa kikatili litafanyika Addis Ababa, Ethiopia,kuanzia tarehe 9-11 May 2016.

Watendaji hao wa kidini wanawakilisha Imani mbalimbali kutoka mataifa tofautikatika mkutano huo ikiwemo Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Cote d'Ivoire, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Ethiopia, Guinea, Kenya, Liberia, Malawi, Nigeria, Rwanda, Somalia, Afrika ya Kusini, Sudan Kusini, Sudan, Tanzania, Uganda na Zimbabwe.

Watendaji hao watashirikiana kwa pamoja katika siku mbili zijazo kuunda mikakati ya kuzuia na kukabiliana na uchochezi , hali kadhalika ubaguzi, uadui na vurugu katika kanda.

Mkutano huo pia utatathimini jumumu la watendaji na viongozi wa dini Afrika katika kuzuia na kupambana na hali ya vijana kuingia kwenye itikadi kali, kuzungumza na wale ambao tayari wamejipenyeza kwenye itikadi kali, ikiwa ni pamoja na wale ambao wamerejea kutroka vitani kwa lengo la kuwajumuisha katika jamii.

Mkutano huo umeandaliwa kwa pamoja na ofisi ya Umoja wa mataifa ya kuzuia mauaji ya kimbari na wajibu wa kulinda, baraza la kimataifa la makanisa na mtandao wa kimataifa kwa ajili ya dini na kuchagiza amani.