Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kimataifa kuhusu suala la Jerusalem kumalizika leo Dakar Senegal

Mkutano wa kimataifa kuhusu suala la Jerusalem kumalizika leo Dakar Senegal

Mji mtakatifu wa kihistoria wa Jerusalemu umesalia kuwa kitovu cha majadiliano yoyote ya suluhu ya suala la Palestina amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon, katika ujumbe wake kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu suala la Jerusalem unaomalizika leo mjini Dakar Senegal.

Katika ujumbe huo ambao umewakilishwa kwa niaba yake na Mohamed Ibn Chambas mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa ofisi ya Umoja wa mataifa Afrika Magharibi UNOWA, Ban amesisitiza ni kwa njia ya majadiliano pekee Jerusalemu itaibuka kuwa mji mkuu wa mataifa mawili na kwa muafaka utakaokidhi pande zote mbili.

Akilaani muendelezo wa mashambulizi baina ya vikosi vya Israel na Wapalestina kwenye maeneo yanayokaliwa ya Ukingo wa Magharibi , ikiwemo Jerusalem Mashariki, ametoa wito kwa pande zote kupunguza mivutano na kuheshimu maeneo matakatifu.

Pia ameitaka Israel kusitisha ujenzi wa makazi ya walowezi akisema ni kinyume cha sheria za kimataifa na ni kikwazo kikubwa kwa machakato wa amani