Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Janga la elimu kwa watoto Ukraine linasikitisha- Bloom

Janga la elimu kwa watoto Ukraine linasikitisha- Bloom

Zaidi ya robo ya watoto ulimwenguni wenye umri wa kwenda shule, wanaishi nchi zilizo kwenye majanga na hivyo kuhatarisha mustakhbali wao. Flora Nducha na ripoti kamili.

(Taarifa ya Flora)

Ripoti hiyo imetolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, hali ambayo imedhihirika pia huko mashariki mwa Ukraine  wakati wa ziara ya balozi mwema wa shirika hilo Orlando Bloom.

Ameshuhudia watoto wakisoma kwenye madarasa yaliyoshambuliwa kwa makombora karibu na eneo la mapigano.

Katika ziara hiyo ya kuhamasisha janga la elimu kwa watoto wanaoishi kwenye mizozo Bloom amesema takribani watoto 580,000 huko Ukraine wanahitaji msaada wa dharura huku zaidi ya 230,000 wamekimbia makazi yao kutokana na mzozo.

 (sauti ya Blooom)

“Unapofikiria kuwa ni asilimia Mbili tu ya misaada ya kibinadamu inaelekezwa kwenye elimu, hii haitoshi kabisa. Watoto wanahitaji elimu kwa maisha yao ya baadaye, watoto wanahitaji elimu ili watangamane kwenye jamii, watambulike na kuwa na mustakhbali wa maisha.”