Baada ya kuhutubia New York, Gertrude awasilisha hoja bungeni Tanzania

4 Mei 2016

Nchini Tanzania, mtandao wa wanahabari watoto uliofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF), umealikwa bungeni mjini Dodoma ili kushiriki mkutano wa kamati inayohusiana na masuala ya watoto.

Miongoni mwa watoto waliozungumza na wabunge ni Gertrude Clement, msichana aliyewakilisha vijana na kuzungumza mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New york, wakati wa utiaji saini mkataba wa makubaliano kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

Amesema ameshuhudia utashi wa serikali katika kushughulikia suala hilo

(sauti ya Gertrude)

Amesema alichozingatia ni umuhimu wa kushirikisha vijana zaidi.

(Sauti ya Gertrude)

Wanahabari watoto wanatarajia kuendelea kuelimisha jamii kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia ripoti zao za redio kote nchini.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud